Wasiliana nasi +255714 738 281

Wasiliana nasi +255714 738 281

Breaking

Tangazo

Saturday, November 14, 2015

Mtumishi wa Mungu ni nani

Tafsiri ya Mtumishi wa Mungu nahisi kama inapindishwa sana katika kizazi hichi tulicho nacho, mtu akisema yeye ni Mtumishi wa Mungu utakuta ana jengo analokusanya watu wanafanya ibada, humo anaombea, anakemea mapepo, anafanya deliverance, anatapisha watu, anaita watu mbele akiomba tu wamama kibao wanaanza kuanguka chini tiiiiiiiiiii, na hata mavazi yake utakuta ni yale ya kuchomekea shati mkanda uko nje, atavaa based kama la wanaijeria, hata ongea yake utakuta sauti kama inakwaruza kwaruza kidogo kwasababu ya kuhubiri kwa sauti kubwa, ya makelele yaani hata kama sio muhimu kupiga makelele hayo. Na kwa bahati mbaya taswira hii ndio imeshaaminika kwa watu wengi kuwa hiyo ndio tafsiri harisi ya Mtumishi wa Mungu, na endapo akitokea mtu haendani na mambo hayo anatiliwa mashaka, haaminiki kirahisi kama ni Mtumishi wa Mungu. Sasa leo nahitaji kuchukua muda mfupi alafu niwapime watumishi ambao hadi record zao ziliandikwa kwenye biblia kama watafit kwenye mizani hii alafu tujiulize kama ni watumishi aka sio watumishi.
Naanza na baba wa imani Ibrahim ambae moja ya ahadi alizopewa na Mungu ndio zinatupatia haki sisi ya kuhesabiwa kama wana na warithi wa ahadi njema alizoaidiwa na Mungu, maana aliambiwa atakuwa na watoto wengi kama mchanga wa bahari na katika yeye mataifa wataitwa kwa jina lake. Ahadi hii ndio inasababisha hadi leo mtu mweusi anaitwa Mtume na Nabii na anasimama kwa ujasiri na kusema Yesu ni Bwana.
Lakini aliyesababisha ahadi hii ikatokea kwetu, Mzee Abraham, katika historia ya maisha yake yote, hajawahi kufungua kanisa na kuwa Mchungaji, wala hajawahi kukemea pepo, wala hajawahi kuombea hata mgonjwa wa mafua na akapona, lakini kwasababu alimsikiliza sana Mungu na kumuamini kama ndio jibu sahihi katika uhitaji wake wa kupata mtoto, japo kuwa hapa katikati alikoseshwa na mke wake hadi akazaa na kijakazi, lakini hakuishikiria dhambi hiyo kama ahadi bali akaendelea kumuamini Mungu kwamba atakuja kupata mtoto kwa mke wake Sara.
Akiwa kama mwanadamu wa kawaida kabisa, kuna wakati alipatwa na mashaka na kuhisi kama mtoto wa mjakazi wake Eliazeri Mdameski ambae alizaliwa katika nyumba yake ndio atakaekuja kurithi mali zake, lakini Mungu aliendelea kumtia moyo.
Abrahamu akaendelea kungoja, miaka ikakatika lakini alingoja kwa saburi hadi siku moja ahadi ile ikatimia. Leo tunamuheshimu Abraham na tunasoma habari zake kwenye biblia, sio kwasababu ya ishara na miujiza aliyoifanya, bali ni kwasababu ya imani aliyokuwa nayo juu ya Mungu wake, sidhani kama amewahi kuvaa bazee la kinaijeria wala kuchomekea na kuvaa mkanda nnje, bali imani yake thabiti mbele za Mungu ndio ilimpatia heshima iliyomjngea historia hadi leo.
Alikadharika Mtumishi wa Mungu Daudi, huyu alikuwa ni Kiongozi wa kisiasa, aliyemuamini sana Mungu, na Mungu akamuonekania kila mahali alipokwenda, ingawa aliishi kama binadamu, kuna mahali alikosea, na kwenye ufalme wake amewahi kupinduliwa lakini Mungu akamsaidia kurudi kwenye kiti chake, yaani ilikuwa ni issue kama iliyomkuta Raisi wa Burundi Pierre Nkurunzinza, lakini Mungu alimpenda sana na alipendezwa sana na moyo wake. Hakuna mahali Daudi amepiga power na kuangusha wanawake chini kwa fireeeeeeeeeeee, wala hakuna mahali amefanyia watu derivarance, na hata unabii alioutoa katika Zaburi juu ya maisha ya Yesu, hakujua kama anatabiri, yeye alikuwa anaandika nyimbo tu kwa ajiri kujifariji na kuwatumainisha watu wake katika Mungu. Ndio maana Yesu aliwaambia Mafarisayo "Kama mnasema mimi ni mwana wa Daudi, mbona Daudi akiwa katika roho aliniita Bwana wangu''.
Ndio maana hatuoni mahali Daudi akijiita Nabii, na hata alipokosea ama alipohitaji msaada alimuita Nabii aje aone kwa ajiri yake, lakini back anaheshimika, na ataendelea kuheshimika kama Mtumishi wa Mungu.
Namalizia na mfano wa mtu mmoja anaeitwa Ayubu, huyu kamanda hakuwa na hekalu analoliongoza, na yeye pia hakuwahi kutoa mtu pepo, wala kupiga power mtu, bali alikuwa ni mfanya biashara na mfugaji, tajiri lakini anaemuamini Mungu sana, kiasi kwamba Mungu akajivuna kwa ajiri yake, na kumuita Mtumishi wangu Ayubu, huyu kamanda alimpenda sana Mungu na kumuamini kuwa Mungu ndio kila kitu kwake, hata alipopata hasara ya kupoteza mali zake, na watoto wake, akiwa kwenye uchungu mkali na maaumivu makubwa ya majipu aliyo nayo mwilini pamoja na maumivu ya moyo, wakati marafiki zake wameungana na mke wake wanamdhihaki na kumuambia Mungu amemuacha, ni afadhali amkufuru Mungu tu ili afe, bado maneno yake yaliendelea kuonyesha kuwa Mungu ndio kila kitu kwake, na hali yeyote njema au mbaya vitapita lakini wema wa Mungu hautapita kamwe. Imani hiyo ndio inasababisha hadi leo hii tubakie na kumbukumbu kuwa amewahi kutokea Mtumishi wa Mungu hapa duniani anaeitwa Ayubu. Ambae hakutetereshwa na hali yeyote bali moyo wake ulimtazama sana Bwana zaidi ya matatizo aliyopitia.
Rafiki yangu unaesoma meseji hii, nataka nikuambe kuwa hata wewe ni Mtumishi wa Mungu, na unaweza kuacha historia kubwa hapa duniani kwa hicho unachokifanya, tena hadi Mungu akajivuna kwa ajili yako. Sio lazima utoe pepo, ufungue kanisa, upige watu power, bali kwa kuisimamia khaki tu, inatosha sana wewe kuitwa Mtumishi wa Mungu.
Iwe ni polisi, hakimu, mwanasheria, daktari, mtoza ushuru, au vyovyote vile, zionyeshe njia za Mungu katika position yako.